Select Page

USHAURI WA THAMANI KAMA DHAHABU KWA WAJASIRIAMALI

USHAURI WA THAMANI KAMA DHAHABU KWA WAJASIRIAMALI

KATIKA MAPATO na UWEKEZAJI:


“Tusiwe na chanzo kimoja tu cha Mapato”. Maana kikikata inakuwa ni kilio kikuu sana.

Pia kama una Biashara hakikisha inakuwa na milango mingi ya kukuingizia kipato.

Pia hata Ujuzi usiwe na kaujuzi kamoja tu. Nyakati huwa zinabadirika na pia unaweza kwenda mazingira ambayo yakahitaji ujuzi tofauti ili uweze kujipatia kipato.

Nakupa mfano. (Mimi mpaka hapa Ninaujuzi wa Ufundi wa mambo ya Kompyuta, lakini pia nimejiongeza natengeneza Websites, na pia kielimu nimesomea Digree ya kilimo. Na bado nikaenda SIDO kupata ujuzi wa kutengeneza sabuni mbalimbali)

Ingawa kujua ni jambo moja lakini kufanyia kazi ujuzi ni jambo lingine; Lakini huwezi kufanyia kazi jambo ambalo hujui. kujua mambo mengi pia ni ulinzi tosha.

USHAURI: Kama unataka uwe na ujuzi wa mambo mbalimbali ya kijasiriamali, Fuatilia SIDO huwa wanatoa mafunzo mbalimbali kwa vitendo kwa ajili ya wajasiriamali. Pia uwe na tabia ya kuhudhuria semina na mafunzo mbalimbali ya kijasiriamali.

Mfano kama unauza bidhaa Fulani basi angali usitegemee duka moja tu. (Ni kweli sio rahisi kuanza ukiwa na maduka mengi. Lakini weka kama lengo la kutokuwa na chanzo kimoja tu cha Pesa aitha iwe ni duka au kazi usitegemee chanzo kimoja tu)

Au kama una Mteja Mmoja mkuwa; basi tusitegemee huyo tu, tuendelee kupiga mbio kutafuta wateja wengine wakubwa pia. Ili kama ukimpoteza mmoja usitikisike kiuchumi

Fikiria mfano huu;

Kama Mtu anakampuni imeajiri watu 20, na wote wanatoa huduma  kwa mteja mmoja na faida ya huyo mteja ndiyo inalipa mishahara na gharama nyingine. Inamaana huyo mteja akipotezwa na kampuni itayumba.

Hivyo iwe una ajira au biashara cha Muhimu bado tusitegemee chanzo kimoja cha Mapato.

KATIKA MATUMIZI:

“Kama unanunua hovyo hovyo vitu visivyo na umuhimu, si muda mrefu utaanza kuuza vitu vya muhimu.”

Umasikini huazia ndani ya akili ya mtu. Hivyo Lazima tuwe na Nidhamu katika Matumizi yetu.

Wale ambao wanaakili za kimasikini huwa wakipata hela huwa hawatulii. Akili zinawasha na wanaishia kuzitumia katika mambo yasio ya msingi. Na zikiisha ndipo anaanza kukumbuka mambo ya msingi.

Mtu mwenye akili za kimasikini hunua vitu vya kitajiri ili aonekane tajiri. Lakini mtu mwenye akili za kitajiri akipata hela akili yake haunza kufikiria uwekezaji kwanza. Na baadaye atatumia matunda ya uwekezaji kununua vitu vya kitajiri. Maana tayari amekuwa tajiri baada ya uwekezaji.

Inatakiwa ujue kutenganisha kati ya matumizi ya Lazima na yasio ya lazima. Kati ya matumizi ya faida na yasiyo na faida. Kati ya matumizi ya haraka na matumizi ambayo ukisubiri hakutakuwa na shida.

KATIKA KUTUNZA PESA

“Usitunze pesa baada ya matumizi, bali kabla ya matumizi itenge pesa ya kuitunza ndipo inayobaki uanze kuitumia”

Lakini ukiangalia wengi sana tunakosea katika hili.

Na njia ya Muhimu hapa ni kuhakikiasha umeipangia Pesa matumizi mazuri kabla haijakufikia. Maana wale ambao wanapata hela bila kuwa walijiandaa kuwa nazo huwa wanaishia kununua vitu na matumizi yasiyo ya lazima.

Mfano: Utafiti unaonesha kuwa asilimia kubwa ya watu wanaoshinda bahati nasibu huwa wanakuwa masikini na kurudi katika hali yao ya kwanza. Sababu kubwa ni kuwa walizipata zile pesa bila kujiandaa kuwa nazo.

Lakini mtu akitengeneza tabia ya kupangia matumizi ya pesa ambayo hana, siku akiipata atajua moja kwa moja aitumie kwenye nini cha Muhimu.

Hii inaisaidia sana kuepukana na matumizi yatokanayo na mizuka (emotional excitement) ya kuwa na pesa

KATIKA KUCHUKUA HATUA HATARISHI – YAANI KUJIRIPUA (ON TAKING RISK)

Sio hekima nzuri kufanya biashara ya majaribio kwa kiasi kukubwa saaana cha Pesa.

Ukifanya hivyo inakuwa kama mtu anayepima kina cha Maji kwa miguu miwili.

Mfano Ukianza moja kwa moja kwa mtaji wa Milioni 100 alafu akapata hasara maumivu yake yatakuwa makubwa sana tofauti na kama ungejaribu kwanza kwa milioni 10

HITIMISHO

Haya ndio baadhi ya mambo ya muhimu kama umeamua kuwa mfanyabiashara au mjasiriamali.

Ila tu ujue kuwa kuyajua haya hakutaleta manufaa kama hutuyafanyii kazi. Na hayo yote yanatakiwa yawe tabia yetu ndani yetu.

Na changamoto mojawapo ni kuwa tabia mala nyingi hazijengwi ndani ya siku moja. Hivyo cha msingi ni kuweka nia ya kuwa na tabia ya kufanya yoote hayo.

Wala usikate tamaa kujiona kuwa hatuwezi. Tufanyie kazi siku hadi siku mwisho wake inakuwa ni tabia yatu ambayo hutahitaji tena nguvu ili ufanye.

About The Author

Ibrahim Nzunda

Ibrahim Nzunda is Self-Employed Owner & CEO of Jimz Technologies Company LTD which he Co-Founded and registered in 2015-Tanzania. He Graduated in 2016 with B.Sc Agronomy at Sokoine University of Agriculture

3 Comments

 1. Michael Paul

  Mawazo Murua Kabisa, hakika kijana akiyafanyia kazi basi ana asilimia kubwa ya kufanikiwa.

  Kazi nzuri sana Ibrahim! Kongole.

  Reply
 2. Anonymous

  Noted brother..

  Reply
 3. Anonymous

  Thanks, be blessed

  Reply

Leave a Reply to Michael Paul Cancel reply

Your email address will not be published.

Subscribe

Share This