
NGUVU YA KUSOMA VITABU KWA MJASIRIAMALI

Kuna kitu cha ajabu nimekiona, kwa wengi walio matajiri au waliofanikiwa kufanya vitu vya ajabu dunaini. Wote wanayo tabia ya Kusoma sana vitabu.
Hebu angalia hii
Na katika hao;
Ni kwa wastani wa vitabu 4 – 12 kwa Mwaka.
Ikimaanisha wengi ndani ya miazi mitatu anakuwa amemaliza kitabu kimoja au Ndani ya kila mwenzi mmarekani anakuwa kasoma kitabu kimoja.
Kumbuka hiyo ni kwa watu wa kawaida tu,
Lakini yako maajabu kwa watu wenye Biashara au kwa watu wenye majukumu makubwa makubwa.
Maana Inaonesha kuwa kwa wastani, CEO wa kawaida anasoma vitabu 4-5 kwa kila mwezi.
Bill Gates, tajiri namba moja duniani, yeye anasoma vitabu 50 kwa mwaka (wastani wa kitabu kimoja kwa wiki).
Warren Buffet, Tajiri namba Mbili duniani, anasoma kurasa 600 kwa siku
(wastani wa vitabu vitatu kwa siku),
Na asilimia 80% ya muda wake kwa siku anautumia kusoma.
Elon Musk, Entreprenuer (mjasiriamali) wa Magari ya Umeme, Mwenye kampuni ya kutengeneza Rockets za Anga, Alijifunza technologia za Rockets na Magari kwa kusoma vitabu.
Na wakati wa utoto wake aliwahi kumaliza Libraly yote aliyokuwa anasoma vitabu,
kiasi kwamba akishia kuimaliza, akasoma na Encyclopedia Britannica (yenye maelfu ya kurasa) yote.
AKILI ZA KIMASIKINI VS KITAJIRI KATIKA KUSOMA
Uchunguzi mwingine unaonesha kuwa;
- 11% ya matajiri ndio husoma vitabu vya burudani (Tamthilia, hadithi, liwaya, Udaku, n.k) , wakati 79% ya watu masikini ndio husoma kwa ajili ya burudani
- 85% ya matajiri husoma vitabu viwili au zaidi vinavyohusuiana na Elimu au Tasnia aliyosomea, au self-improvement books kwa mwezi, lakini ni 15% ya masikini hufanya hivyo.
- 94% ya matajiri husoma habari, machapisho (magazeti, Makala, Kwenye mitandao, n.k), wakati ni 11% tu ya masikini hufanya hivyo.
Kwahiyo;
KATIKA KUFANIKIWA; USOMAJI VITABU NI MOJA YA NGUZO AMBAYO HAINA MBADALA