fbpx

Select Page

UNATAKA KUFUNGUA KAMPUNI? HIZI NI FAIDA ZA KUFUNGUA KAMPUNI

UNATAKA KUFUNGUA KAMPUNI? HIZI NI FAIDA ZA KUFUNGUA KAMPUNI

Kama una malengo makubwa nakuomba uwaze kuwa na kampuni hata kama utashindwa kwa sasa ila baadae jitahidi.

Kufungua kampuni sio lazima uwe na mtaji, na gharama za kufungua ni ndogo sana. Angalia hapa gharama zake zilivyoanishwa na Brela. Lakini faida ya kufungua kampuni ni kubwa sana sana na ni muhimu sana.

Kwa haraka haraka, ukiwa na kampuni;

 1. Kodi inatozwa kwenye faida utakayopata (tena hata faida yenyewe unakatwa kodi yake ile faida uliyoshindwa kuitumia). Mfano. Kama niliuza mauzo ya Mil 100, na humo nilipata faida Mil 30, lakini nikanunua gari ya kampuni mil 25, basi kodi nitakatwa kwenye Mil 5.  Kwa Mtu binafsi angekatwa zaidi ya mil 10
 2. Makadirio ya kodi utafanya mwenyewe
 3. Inatambulika kisheria(legal entity).
 4. Kama una hasara hutakiwi kulipa kodi
 5. Huwezi kurisisha Kazi ya kuajiriwa, bali unaweza kurithisha Kampuni. Na pia ni rahisi kuepuka migogoro ya mirathi kama una kampuni kuliko mali binafsi
 6. Ni rahisi kukopesheka kama biashara iko vizuri au kuaminika na makampuni mengine.
 7. Ukiwa na kampuni ni rahisi kutumia mtaji wa kampuni nyingine pasipo mkopo. Yaani ni rahisi kupewa bidhaa na kampuni nyingine pasipo kulipa kwanza kwa makubariano ya kulipa baada ya kuuza (Credit facility).

Kwa hiyo ukiwa na kampuni wimbo wa sina mtaji unapotea na pia unaingia kwenye uwanja wa kula vinono. (Mfano huwezi kupata tenda ya kutengeneza barabara kama wewe sio kampuni).

KIUNDANI: FAIDA ZA KUFUNGUA KAMPUNI

 • Kuwa na kampuni kunakuwezesha kuingia katika biashara kubwa kubwa ambazo hawezi kupewa mtu binafsi (contract au tenda) na pia inafungua mlango na trust kuweza kushirikiana  na makampuni mengine, kwa kuwa makampuni yanaamini na kufanya biashara na makampuni badala ya mtu binafsi.
 • Pia ukiwa na kampuni ni rahisi kutumia mtaji wa kampuni nyingine pasipo mkopo. Yaani ni rahisi kupewa bidhaa na kampuni nyingine pasipo kulipa kwanza kwa makubariano ya kulipa baada ya kuuza (Credit facility).

Mfano kama umepewa tenda ya kusupply Mifuko 1000 ya mbolea kwenda kampuni X ya kilimo, Basi ukiwa na kampuni yako ni rahisi kampuni Y inayozalisha Mbolea hizo kukupa mzigo mbolea ukasupply kwa mteja X; na wewe ukawalipa baada ya kupewa hela. (Yaani unatumia mtaji wa manufacturer wewe kufanya biashara hata kama huna mtaji).

 • Ukiwa umesajili kampuni unakuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kupata ushirikiano na hao walengwa wako kwa haraka zaidi maana wanakuwa wanaongea na kampuni na sio mtu binafsi. hii ni Kama una wazo la kutafuta wafadhili wa biashara yako.
 • Kuna makato madogo ya kodi kwasababu kampuni unakatwa kodi kiasi cha faida ulichoshindwa kutumia na sio kiasi cha mauzo yote. Yaani unakatwa kodi baada ya matumizi na sio kabla ya matumizi.

Mfano: Kama una mauzo ya Milioni 100; basi ambaye hana kampuni atakatwa zaidi ya Milioni 10 au zaidi. Lakini  kampuni unakatwa kodi kiasi cha faida tu ambacho hujatumia. Yaani kama kwenye mauzo ya Milioni 100 ulikuwa na faida ya Milioni 30;  lakini ukaitumia hiyo faida kwa matumizi ya kampuni (Mfano kununua gari ya kampuni, kuwekeza, n.k) baadaye ukabaki na Milioni 5, basi unakatwa kodi kwenye hiyo Milioni 5. Kitu ambacho hakipo kwa Mtu binafSi.

 • Chini ya kampuni moja unaweza kufanya biashara nyingi tofauti, ili linawezekana kupitia kukata leseni tofauti za biashara (business license) kulingana na shughuli unazotaka kufanya. Yaani kampuni moja inaweza kuwa na leseni za biashara zaidi ya moja.
 • Ukiwa na kampuni ni rahisi kumrithisha ndugu, mtoto au mtu wako wa karibu hizo biashara kupitia hiyo kampuni. Ukifanya biashara kama mtu binafsi inamaanisha wewe ndiyo mmiliki pekee wa hiyo biashara, yaani hautaweza kummilikisha mtu mwingine.
 • Pia unakuwa na nafasi ya kutofautisha mali zako binafsi na mali za kampuni. Hii itakusaidia pale ambapo imetokea kampuni yako inadaiwa, basi deni hilo halitafika kwenye mali zako binafsi ambazo hazimilikiwi na kampuni

SIKU UKIHITAJI KUFUNGUA; TUNATOA HUDUMA YA KUFUNGUA KAMPUNI

 1. Kuandaa MEMART. (Memorandum of Association and Articles of Association)
 2. Name search na kusajili BRELA
 3. Kukusaidia Mambo ya TRA na Manispaa
 4. MAMBO YA MPANGILIO WA MAHESABU (record keeping system) NA ACCOUNTING SOFTWARE YA KUTUNZA KUMBUKUMBU
 5. Kutengeneza Company Website or official company email (bila website). Pamoja na kufanya setup nzima ili muweze kuzitumia proffesionally bila shida.
 6. Na kuwapa mikataba ya wafanyakazi kama mtapanga kuajiri au ili kuitumia wakati wa kuajiri. (Ready made contracts)
 7. Kuwasiadia/kuwaongoza usajili wa bank account ya kampuni, NSSF, NA WCF (wokers compassion fund)

KUIJUMLA WE HELP TO REGISTER, ESTABLISH AND TO MAKE YOUR COMPANY RUN PROFESSIONALLY

Mawasiliano

0625 992 014 (Call/Whatsapp/text)

Info@wajasiriamali.co.tz

Info@kingbest.co.tz

About The Author

Ibrahim Nzunda

Ibrahim Nzunda is Self-Employed Owner & CEO of Jimz Technologies Company LTD which he Co-Founded and registered in 2015-Tanzania. He Graduated in 2016 with B.Sc Agronomy at Sokoine University of Agriculture

19 Comments

 1. Luis Baraka

  Just skimmed through,
  Nice Article!!!
  Please make it available to remote people, use familiar terms to them e.g. instead of calling it a ‘company’ (scary term to many) call it a ‘registered business’ if applicable!
  I agree with you, a formal registered agriculture company which makes millions per month pays less tax than a shop winch makes half the profit.

  Reply
 2. Dilma Line

  Hongera brother. hongera kwa kuweka hizi makala kwa kiswahili ila kwa kuongeza tu ungekuwa unaweka picha. Picha zinasema maneno mengi zaidi. kwa mfano ukitamka term kama kampuni unaweza kuweka mfano wa Jimz Tech na picha yake, au mifano ya accounting softwares (picha) nk. But all in all hongera sana na soon nitakutembelea kwa ajili ya kubadilishana mawazo.

  Reply
 3. Anonymous

  Thanks brother for sharing. I have a thing with understanding how things works. Hii itanisaidia sana.

  Reply
 4. Eric Urio

  KAZI NZURI SANA UNAYOFANYA KAKA, NAKUPONGEZA SANA SANA. KWA MAKALA ZA MAANA KAMA HIZI

  Reply
  • Ibrahim Nzunda

   Nashukuru sana mkuu.. Karibu sana…

   Reply
   • Anthony Sendi

    Asante kwa ushauri,uko wapi niweze kufka ofcn kwenu ili kujua Namba ya kufungua?!

    Reply
    • Ibrahim Nzunda

     Tuko Morogoro. Wasiliana nasi via 0754210627 au 0625992014

     Reply
 5. Sheddy Ng'wavi

  Nashushukuru ndugu Ibrahim Kwa makala uliyoiweka hapa nimeipitia nimeelewa uzuri wa kuwa na kampuni.Sasa Mimi ni Fundi Umeme halafu sina mtaji sasa ningetaka kujua gharama za kusajiri kampuni japo umesema ni ndogo je Tsh ngapi.nipo Njombe

  Reply
  • Ibrahim Nzunda

   Habari.

   Ufundi ni huduma. Na huduma huwa haihitaji mtaji.

   Ndio maana Brela wameruhusu mtu kufungua kampuni kuanzia mtaji mdogo wa 20,000

   SO TATIZO LABDA LINAWEZA KUWA KWENYE GHARAMA ZA USAJILI .. LAKINI SIO MTAJI..

   Reply
   • Sheddy Ng'wavi

    Asante ndugu vipi sheria ya kodi inasemaje kuhusu huduma za ufundi kama kampuni?

    Reply
    • Ibrahim Nzunda

     Naomba tuwasiliane whatsapp. Kwa ajili kurahisisha zaidi. 0625992014

     Reply
  • Ibrahim Nzunda

   Kwa mtaji kuanzia 20,000 ~1 milion Brela wameweka gharama za usajili jumla (registration fee, stamp duty fee, na filling fee) jumla ni 167,200

   Reply
 6. Anonymous

  Habari binafsi ninashauku pia yakufungua kampuni sijui kwa hapa mwanza mnapatikana wapi??

  Reply
  • Ibrahim Nzunda

   Habari,

   Usajili unafanyika online. check Brela.go.tz

   pia sisi tuko Morogoro. So kwa jinsi hiyo tunaweza kusaidia watu kusajili kutoka mikoa yoyote maana usajili wote ni online..

   Reply
 7. Anonymous

  good adea

  Reply
 8. Anonymous

  keep here contact plz

  Reply
 9. Mapisha Mkendi

  Asante sana Ibra. Tutakuona siku za usoni kwa mengi. Hongereni kwa ufafanuzi na mwongozo mzuri pia. Pamoja sana

  Reply
 10. kaayaforhealth

  je ili kufungua kampuni ni lazima uwe na ofisi?

  Reply

Trackbacks/Pingbacks

 1. FAIDA NA JINSI YA KUSAJILI BUSINESS NAME (JINA LA BIASHARA) | Wajasiriamali.co.tz - […] UNATAKA KUFUNGUA KAMPUNI? HIZI NI FAIDA ZA KUFUNGUA KAM… USHAURI WA THAMANI KAMA DHAHABU KWA WAJASIRIAMALI How to register…

Leave a Reply

Subscribe

Share This
%d bloggers like this: