fbpx

Select Page

Umuhimu wa Business Email kwenye biashara yako na jinsi ya kuwa nayo

Umuhimu wa Business Email kwenye biashara yako na jinsi ya kuwa nayo

Business email; mfano info@kingbest.co.tz, ni email za kiofisi kwa ajili ya mawasiliano yote muhimu kwa ajili ya biashara yako au kampuni yako.

Mtu ambaye hatumii email za namna hii mara nyingi anaonekana hayuko professional bado.

Faida yake kuu ni kuongezea uaminifu na kuonesha kuwa uko serious na biashara au kampuni yako. Sasa kama unatumia gmail ni rahisi mteja au mtu kujua kuwa hauko serious.

Na mara nyingi wateja wa biashra kubwa kubwa mara nyingi huwa hawawapi kazi watu wasio na business email

Business email inasaidia mteja kupata uhikaka na kujua kuwa anawasiliana na mtu sahihi kutoka kwenye kampuni husika. Tofauti na ukiwa unatumia email ya kawaida ambayo haina jina la biashara yako.

Hivyo inakuwa rahisi mteja kukuamini na kufanya biashara nawe kwakuwa inasaidia kuepuka utapeli. Maana unatumia official email, ni rahisi mteja kukuamini kuwa unafanya biashara halali na sio miongoni mwa matapeli.

Pia inasaidia kuonesha kuwa uko professional , yaani ni mtu wa kufanya biashara kwa viwango vya ubora (professionalism)

GHARAMA ZA KUPATA BUSINESS EMAIL

Kwa Tanzania, kuna watoa huduma wengi waambao unaweza kununua domain name ya biashara yako pamoja na kufanya hosting ya email.

Kwa uzoefu wetu tumeona Yatosha.com na Extreme Web technologies na Kilihost Kwa hawa wako reliable na hatujapata usumbufu kwao.

Kupata business email kuna gharama mbili.

 1. Kununua domain name mfano kingbest.co.tz
 2. Kununua hosting space

Domain name unaweza kuinunua HAPA au HAPA Hawa ndio gharama zao ziko ndogo ziadi, na hawana usumbufu. Domain name jumla ni TSH 25000 kwa Mwaka

Hosting kwa kwa makampuni ya TZ bado sijaona wenye gharama nafuu ukiringanisha na makampuni makubwa ya nje. Hivyo nashauri domain nunua Tanzania na hosting unaweza kunua ya 20GB, unlimited email, via NAMECHEAP .

Hawa nao gharama zao ni ndogo pia ukilinganisha na wengine wengi. Namecheap ndio tunaowatumia kuhost website zetu zote. Utachagua Stellar Hosting plan- Annual Plan kwa mwaka wa kwanza ni $18.44 /yr , Renewal baada ya mwaka kuisha ni $33.88/yr

Hivyo basi, kununua Domain ni Tsh 20,000, na kununua hosting ni $18.44 . Inamaana ukiwa na hicho kiasi unaweza kuwa na business email yako na kuanza kula matunda ya wewe kufanya biashara professionally.

JE UNAHATIJA MSAADA?

Kama ukitaka msaada wa kufanyiwa setup ya email zako usisite kututafuta.
Whatsapp link ni BOFYA HAPA kuchat nasi moja kwa moja via whatsapp. PIA; Tunafanya consulting (kusaidia) kusajili kampuni au business name yako brela kwa HARAKA NA UFANISI zaidi. Hivyo siku ukihitaji usisite kututafuta pia.

Imeandikwa na

About The Author

Ibrahim Nzunda

Ibrahim Nzunda is Self-Employed Owner & CEO of Jimz Technologies Company LTD which he Co-Founded and registered in 2015-Tanzania. He Graduated in 2016 with B.Sc Agronomy at Sokoine University of Agriculture

9 Comments

 1. Anonymous

  Ahsante kwa kuturudisha school hapa umenitoa ujinga kaka.
  Barikiwa sana

  Reply
 2. Anonymous

  Ahsante kwa kuturudisha school hapa umenitoa ujinga kaka.
  Barikiwa sana

  Reply
 3. Deus Amos Jasson

  Okay, thanks for everything. I will keep in touch.

  Reply
 4. Anonymous

  Nimefrahi sana kukutana nanyi maana siku nyingi najiuliza nawezaje kufungua website yangu kwaajili ya kuandaa makala mbali mbali za kiafya na kuzianika mtandaoni

  Reply
 5. Alfred

  You give what we need,thank you so much.I will come to you in business soonest

  Reply
   • Anonymous

    Nimefurahi sana kupata elimu juu ya umuhimu wa kuwa na company email.
    Nitawatafuta

    Reply

Leave a Reply

Subscribe

Share This
%d bloggers like this: