fbpx

Select Page

KWANINI NI MUHIMU KUWA NA KAMPUNI?

KWANINI NI MUHIMU KUWA NA KAMPUNI?

Lengo na idea ya kufungua kampuni ilikuwa ni ili kumlinda mfanyabiashara

Kampuni ni kama mtu, yenyewe inauwezo wa kumiliki mali, kudai, kushtaki, kudaiwa na kushtakiwa

mfano: kampuni ikipata hasara na kudaiwa, basi mdai ataidai kampuni tu na kama ni mali zitauzwa za kampuni tu.

Lakini mtu ambaye hana kampuni atadaiwa yeye na nyumba yake ya kukaa na kila mali ambayo inaweza kutumika kulipa deni ambayo iko chini ya jina lako.

Pia kampuni kwa kuwa inaongozwa kimpangalio, basi inakuwa ni system. Hivyo watu wanakuwa wanaamini zaidi system kuliko mtu bianafsi.

Kwahiyo kazi professional au tenda (zabuni) kutoka kwa wateja walio serious huwa zinapewa kampuni badala ya mtu binafsi.

Pia kampuni kwa kuwa ni system inakuwa ni rahisi kurithisha.
Yaani, mmiliki akifa ni rahisi kurithisha system kuliko kulithisha biashara ambayo ilikuwa inaendeshwa kienyeji.

Kwahiyo inasaidia katika udumuji wa mali zilizochumwa na founders (waanzilisi). Na kwakuwa iliundwa kumlinda mmiliki, inasaidia pia kwenye mambo ya kodi.

Yaani, kampuni inalipa kodi kutoka kwenye faida (profit) na sio kwenye mauzo(revenue).

kwa sheria zilizopo kampuni ikipata hasara inaweza isilipe kodi (kama inao ushahidi wa hasara ) lakini mtu binafsi hana hiyo faida. (hizi ni miongoni mwa Sheria ambazo makampuni ya madini huwa yanatumia sana).

Kuhusu kodi, Kodi hawakati kutokana na ukubwa wa mtaji, Wala hawaangalii mtaji ili kujua kiasi cha kodi cha kulipa.

Pia kampuni moja inaweza kufanya biashara tofauti tofauti nyingi sana kuliko mtu binafsi mwenye business name. Na kampuni moja naweza kumiliki makampuni mengine pia.

Kitu kinachotakiwa ni mtu mwenye kampuni kuwa “smart” kwa kutunza kumbukumbu za biashara anazofanya

Yaani kutunza taarifa za mauzo, manunuzi, na matumizi. Wale wanaotaka kufanya biashara kiholela bila daftari ndio huwa hawataki mambo ya kuwa na kampuni. Ingawa kwa kufanya hivyo wanajifungia fursa na kujitoa kwenye uwezekano wa kula kazi kubwa kubwa.

Jiulize swali; Uliwa kumuona mtu tajiri sana ambaye hana kampuni? Sana sana mtu anayefanya biashara kiholela bila usajili akiwa tajiri ataishia kuchunguzwa na kudhaniwa labda anafanya biashara haramu.

Pia ni rahisi kushirikiana na makampuni mengine MFANO Kuchukua bidha kwa njia ya mali kauli (credit) kuliko mtu binafsi. Hii bado ni faida ya trust.

Kwakuwa inafahamika ni vigumu kampuni kukimbia na mali za watu, lakini ni rahisi mtu ambaye hana usajili wowote kukimbia na mali za watu.
___________________________


Tunafanya consulting (kusaidia) kusajili kampuni au business name yako brela kwa HARAKA NA UFANISI zaidi. Hivyo siku ukihitaji usisite kututafuta. Whatsapp link ni BOFYA HAPA kuchat nasi moja kwa moja via whatsapp

Imeandikwa na

About The Author

Ibrahim Nzunda

Ibrahim Nzunda is Self-Employed Owner & CEO of Jimz Technologies Company LTD which he Co-Founded and registered in 2015-Tanzania. He Graduated in 2016 with B.Sc Agronomy at Sokoine University of Agriculture

Leave a Reply

Subscribe

Share This