fbpx

Select Page

kampuni binafsi ya Ulinzi; Jinsi ya kufungua na kupata kibali chake

kampuni binafsi ya Ulinzi; Jinsi ya kufungua na kupata kibali chake

Kama unao uzoefu kwenye mambo ya Ulinzi, au umepitia mafunzo yoyote ya mambo yanayohusiana na kazi hiyo. Basi ni vyema ukageuza huo ujuzi au uzoefu kuwa Biashara. Na ni rahisi tu.

Hatua ya kwanza ni kuandaa jina zuri la kipekee(uniquee) kwa ajili ya kampuni yako. Na hilo jina liwe na neno “Security” au “security services”. Mfano Wajasiriamali Security Services Limited. Hilo jina lifanyie clearance Brela (kuhakikisha kuwa hakuna mtu mwingine aliyesajili jina kama hilo )

Unaandaa Memorandum and Articles of association(Memart), hiyo memart iwe na mambo ya ulinzi tu. Isichanganywe na biashara nyingine isipokuwa zile za mambo ya ulinzi tu.

MAHITAJI YA KUSAILI KAMPUNI YA ULINZI BRELA

 1. Namba za Nida (kila mtu yake)
 2. TIN numbers (Kila mtu yake,TIN yoyote aliyonayo kwa jina lake)
 3. Phone, email, (kila mtu yake)
 4. P. O. Box zenu.
 5. Mahali mnapokaa kila mtu

NB: kazi ya tin ni kama kazi ya Namba ya nida. kwa ajili ya usajili sio biashara. ya biashara utatumia tin ya kampuni baada ya kusajili kampuni.

Hivyo kama huna tin APPLY NON-BUSINESS TIN Via ots.tra.go.tz

P. O. BOX kama hauna tumia hata ya shule, kanisa au msikiti au ya ndugu.

Idadi minimum ni wawili (wewe na mwenzako mmoja). NDIVYO SHERIA INATAKA) au wakizidi haina shida.

Kwahiyo kama wewe ndiye mmiliki mkuu basi Tafuta mtu mpatie chini ya 1% shares ili wewe umiliki zaidi ya 99% (mke/mume/ndugu/rafiki/mtoto wako/ n.k).

KAZI YA UPANDE WETU NI👇🏾👇🏾 (Hii ni kama ukiamua kututumia sisi kukusaidia hii kazi ya usaili wa kampuni, lakini kama unaweza basi unaweza kufanya hata mwenyewe)

 1. Kuandaa Memorandum and articles of association
 2. mwanasheria
 3. kujaza forms zote zinazotakiwa
 4. na kufanya application online kwenye mfumo wa Brela ors

JINSI YA KUPATA KIBALI CHA BIASHARA YA ULINZI KWA IGP

Haya maelezo ya namna ya kupata kibali yasikutishie, sio magumu ni suala la kuafata tu protocals walizoziweka. Hivyo kwa urahisi sana kupata pa kuanzia we unaenda tu kwa Mkuu wa polisi wilaya(ambapo utaweka ofisi ya kampuni yako). Hapo mambo mengine yanakuwa rahisi.

MAHITAJI ILI KUPEWA KIBALI CHA ULINZI

Muombaji anatakiwa kuandika barua ya maombi.  Barua hiyo eilekezwe kwa lnspekta Jenerali wa Polisi kupitia kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa husika na kupitia kwa (cc) Mkuu wa Polisi Wilaya husika. Vilevile ipitie katika serikali za mtaa ambapo ofisi inapatikana. Barua ioneshe ofisi ilipo (Physical Address) mtaa na namba ya nyumba.

Barua hiyo inatakiwa kwa na viambatanisho vifuatavyo;­

 1. Memorandum and Articles of Association (liyosainiwa na nwanasheria/Hakimu). lnayohusu masuala ya ulinzi tu.
 2. Picha passport size 4 pcs kila mkurugenzi aliyeandikwa kwenye Memorandum and Articles of Association.
 3. Curriculum Vitae za kila mkurugenzi aliyeandikwa kwenye Memorandum and Articles of Association.
 4. Nakala ya kitambulisho cha kila mkurugenzi. Kitambulisho kiwe cha utaifa au cha kupigia kura au hati ya kusafiria.
 5. Bank statement ya mmoja wa wakurugenzi kuonesha uwezo wao wa kumudu jukumu hili la ulinzi.
 6. Police clearance certificate/taarifa ya uchunguzi wa alama za vidole za kila mkurugenzi aliyeandikwa kwenye Memorandum and Articles of Association.

____

JE UNAHITAJI MSAAADA?

Tunafanya consulting (kusaidia) kusajili kampuni au business name yako brela kwa HARAKA NA UFANISI zaidi. Hivyo siku ukihitaji usisite kututafuta. Whatsapp link ni BOFYA HAPA kuchat nasi moja kwa moja via whatsapp

Imeandikwa na

About The Author

Ibrahim Nzunda

Ibrahim Nzunda is Self-Employed Owner & CEO of Jimz Technologies Company LTD which he Co-Founded and registered in 2015-Tanzania. He Graduated in 2016 with B.Sc Agronomy at Sokoine University of Agriculture

Leave a Reply

Subscribe

Share This