fbpx

Select Page

FAIDA NA JINSI YA KUSAJILI BUSINESS NAME (JINA LA BIASHARA)

FAIDA NA JINSI YA KUSAJILI BUSINESS NAME (JINA LA BIASHARA)

MAANA YA BUSINESS NAME

Kuna utofauti kati ya kampuni na jina la biashara (business name). Jina la biashara ni jina la utambulisho ambalo umeamua biashara yako ifahamike na kuitwa.

Mfano ni majina ambayo wengi wanaandika kwenye maduka yao. Yale ni majina ambayo wameamua duka na biashara zao zitambulike

Hivyo. Business name ni jina tu la kufanyia biashara (Brand name).

Kampuni ni kama mtu, ina uwezo wa kumiliki mali, kudai na kudaiwa. Jina la kampuni na kampuni ni kitu kimoja, maana kampuni hauwezi kuwepo bila kupewa jina ambalo itasajiliwa na kutambuliwa kwa hilo. Faida za kampuni utaangalia hapa

Sasa wenye mamlaka ya kusajili majina kwa mujibu wa sheria ni Brela. Na usajili unafanyika kwa njua ya mtandao online. Check Brela

FAIDA ZA BUSINESS NAME

Ukisajili hilo jina unakuwa umelifanya jina la biashara yako litambulike kisheria na kuwa rasmi (kurasimisha).

Pia inakusaidia kuweza kuzuia mtu mwingine kutumia jina lako isivyohalali. Mfano ni hatari kulikuza jina ambalo hujasajili, au jina la bidhaa maarufu bila kulisajili hilo jina ili kulinda mtu mwingine adandie brand yako au bidhaa yako.

Kwasababu jina linakuwa rasmi, unaweza kufungua account ya bank yenye hilo jina lako ulilosajili. Hii inasaidia katika uaminifu mtu akiona analipa kwenye account yenye jina la biashara.

Mtu mmoja au kama mko kikundi mnaweza kusajili jina la biashara, na kikundi chenu kikafahamika kwa hilo jina kiasi kwamba hata account ya bank mnaweza kufungua kwa hilo jina.

Pia kama mnataka mikopo kwenye taasisi za fedha huwa wanahitaji usajili wa namna hii kama ushahidi kuwa ninyi ni kikundi halali na sio kikundi hewa ambacho hakijasajiliwa popote.

GHARAMA ZA USAJILI

Kujua gharama angalia brela.go.tz, sehemu ya Business name, the angalia kipengele cha fee structure. Utaona wameweka gharama ya usajili jina brela ni 20,000 (elfu ishirini)

MAHITAJI ILI KUSAJILI

Kwa business name vinavyo vinavyohitajika ni;

  • 1. Namba ya Nida
  • 2. namba ya simu
  • 3. email
  • 4. P. O. Box
  • 5. Location (mahali)

SIKU UKIHITAJI KUSAJILI JINA AU KAMPUNI

Tunafanya consulting (kusaidia) kusajili business name yako brela kwa HARAKA NA UFANISI zaidi. Hivyo siku ukihitaji usisite kututafuta. Whatsapp link ni BOFYA HAPA kuchat nasi moja kwa moja via whatsapp

Mawasiliano

About The Author

Ibrahim Nzunda

Ibrahim Nzunda is Self-Employed Owner & CEO of Jimz Technologies Company LTD which he Co-Founded and registered in 2015-Tanzania. He Graduated in 2016 with B.Sc Agronomy at Sokoine University of Agriculture

1 Comment

  1. richard

    oky just fine, nahitaji kusajil jina ya biashara yangu kutakuwa na kodi zozote za kulipia kila mwaka? ukiachan na hiyo ef ishirini nitakayo toa?

    Reply

Leave a Reply

Subscribe

Share This
%d bloggers like this: